Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Kamati ya Hafla ya Kubadilisha Bendera katika Haram Takatifu ya Abbasiyya imetangaza kukamilika kwa maandalizi yake kwa ajili ya kuandaa hafla ya kubadilisha bendera ya kuba ya Haram Tukufu ya Hadhrat Abul-Fadhl al-Abbas as, ikiwa ni ishara ya kuingia kwa miezi ya Muharram al-Haram na Safar al-Khayr.
“Hajj Kadhim Abadah”, mwenyekiti wa kamati hiyo, alisema: “Kama ilivyo desturi kila mwaka ambapo huundwa kamati maalumu ya kusimamia hafla ya kubadilisha bendera, kamati hii imekamilisha maandalizi yote maalumu kwa ajili ya kuendesha hafla ya kubadilisha bendera ya kuba ya Haram ya Hazrat Abul-Fadhl al-Abbas (as). Pia imeandaa sehemu maalumu na mapambo ya kipekee yanayolingana na mazingira na hisia za tukio la Karbala.”
Aliongeza pia: “Hafla hii itafanyika jioni ya Jumanne tarehe 16 Juni 2026 (26 Khordad 1405), ikiwa ni ishara ya kuanza kwa mwezi wa Muharram al-Haram na kuzipokea siku za huzuni na maombolezo ya msiba wa Hadhrat Aba Abdillah al-Husayn (as) na Ahlul-Bayt wake (as).”
Maoni yako